1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Israel laamuru maelfu kuondoka maeneo ya Gaza

8 Agosti 2024

Jeshi la Israel limeamuru kuhamishwa tena kwa watu wengi wanaoishi katika maeneo ya karibu na Khan Younis kusini mwa Gaza.

https://p.dw.com/p/4jGE2
Hali ya Ukanda wa Gaza
Hali ya Ukanda wa Gaza.Picha: Bashar Taleb/AFP

Limesema askari wake watafanya hivi karibuni operesheni ya kujibu kombora la Wapalestina.

Khan Younis ambao ni mji wa pili kwa ukubwa katika Ukanda wa Gaza, umeharibiwa pakubwa kutokana na operesheni za majeshi ya anga na ardhini mapema mwezi huu.

Mivutano ya kikanda imeongezeka tangu kiongozi wa kisiasa wa wanamgambo wa Hamas Ismail Haniyeh alipouawa Julai 31 nchini Iran katika kile kinachodhaniwa kuwa ni shambulizi la Israel.

Kuna hofu ya kufanyika mashambulizi ya kulipiza kisasi. Wakati huo huo, mataifa ya Magharibi yamelaani matamshi ya Waziri wa fedha wa Israel Bezalel Smotrich mwenye siasa kali za mrengo wa kulia aliyesema kuwa ni "haki" kusababisha njaa kwa Wapalestina milioni mbili huko Gaza hadi watakaporejeshwa nyumbani mateka ambao bado wanashikiliwa na kundi la Hamas.