JERUSALEM:Fischer kukutana na Qorei na Sharon Waziri wa mambo ya nje ...
17 Desemba 2003wa Ujerumani Yoschka Fischer anatazamiwa kukutana na Waziri Mkuu wa Palestina Ahmed Qorei na Waziri Mkuu wa Israel Ariel Sharon katika mkondo wa mwisho wa ziara yake ya Mashariki ya Kati. Hata hivyo Fischer ambaye ni mwanadiplomasia wa ngazi ya juu kabisa kumtembelea Qorei tokea aingie madarakani hapangi kukutana na kiongozi wa Palestina Yasser Arafat. Inasemekana kwamba Fischer ameshajiishwa na mikutano yake ya hivi karibuni na Rais Hosni Mubarak wa Misri na Amre Moussa Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu na anataraji kwamba mchakato wa amani uliokwama unaweza kufufuliwa. Gazeti moja la Israel limeripoti kwamba Sharon yumkini leo akatangaza kuanza tena kuvunjwa kwa makaazi ya walowezi ya Kiyahudi juu ya kwamba kuna repoti za kutatanisha kwamba yumkini Israel ikaanza kuchukuwa hatua kadhaa za upande mmoja iwapo juhudi za kuanza tena mazungumzo na Wapalestina zinashindwa.