JERUSALEM: Wayahudi wanaopinga mpango wa kuondoka Gaza wafanya maombi maaulumu
11 Agosti 2005Matangazo
Maelfu ya waisraeli wanaopinga mpango wa kuyaondoa makazi ya wayahudi kutoka ukanda wa Gaza wamefanya maombi maalumu katika mahala patakatifu kabisa pa dini ya kiyahudi. Watu elfu 50 walikusanyika katika ukuta wa magharibi mjini Jerusalem na kuomba mpango huo unaotarajiwa kuanza wiki ijayo usifaulu.
Katika tukio la kushangaza rais wa Israel, Moshe Katsav, amelihutubia taifa akiwaomba wakaazi wa Gaza waisamehe serikali kwa mpango huo wa kuyaondoa makaazi ya ya walowezi wa kiyahudi kutoka Gaza. Rais Katsav pia amewataka waisareli wote wawe na umoja na wala wasijiingize katika mapigano na walinda usalama wakati wa kuondoka kutoka ukanda wa Gaza.