1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem. Viongozi wa Israel na Palestina wakubaliana kukutana.

3 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEVW

Waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon amezungumza na kiongozi wa mamlaka ya wapalestina Mahmoud Abbas na viongozi hao wawili wamekubaliana kukutana hivi karibuni. Sharon na Abbas walitarajiwa kukutana Jumapili, lakini mkutano wao ulifutwa baada ya Israel kuanza mashambulizi yake dhidi ya wapiganaji wa Kipalestina wiki iliyopita.

Katika taarifa , ofisi ya Sharon imesema kuwa viongozi hao wawili wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wao na kufanyakazi kwa pamoja kuendeleza hatua za kuleta amani.

Hakuna tarehe iliyopangwa kwa ajili ya mkutano huo.

Israel imesitisha kampeni yake ya wiki nzima ya mashambulizi dhidi ya ukanda wa Gaza leo Jumapili baada ya makundi ya wapiganaji ya Hamas na Islamic Jihad kutangaza kumaliza mashambulizi yao ya maroketi dhidi ya Israel.