1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM. Sharon aitaka Palestina kukomesha machafuko.

21 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFKv

Waziri mkuu wa Israel, Ariel Sharon, ametaka wapalestina wakomeshe ugaidi kabla kutekelezwa kwa mpango wa amani ya mashariki ya kati unaodhaminiwa na Marekani. Akizungumza katika redio ya kitaifa, Sharon alisema hatarajii tu kukomeshwa kwa ugaidi bali pia uchochezi wa machafuko. Mpango wa amani unalenga kuunda taifa huru la Palestina pamoja na taifa salama la Israel.

Jeshi la Israel limeanza kuondoa vifaa vyake ambavyo havitumiki kutoka mkanda wa Gaza. Hii ni hatua ya kwanza katika mpango wa kuyaondoa makazi ya walowezi wa kiyahudi kutoka eneo hilo, ambalo Israel imelikalia kwa miaka karibu 40. Wanajeshi wa Israel na wayahudi 8,000 wanatarajiwa kuondoka Gaza katikati ya mwezi Julai mwaka huu.

Lakini serikali inajadili uwezekano wa kuuahirisha mpango huo ili kuzuia kufanyika sambasamba na kipindi cha maombelezo ya kiyahudi. Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amesema yuko tayari kushirikiana na Israel kuhakikisha mpango huo unafaulu kwa amani na utulivu.