1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM. Mwanajeshi wa Israel asimamishwa kazi.

5 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFGR

Jeshi la Israel leo limemsimamisha kazi afisa wake aliyekuwa akikiongoza kikosi ambacho kiliwaua vijana wawili wa kipalestina kwa kuwapiga risasi wakati wa maandamo katika mji wa Beit Laqia, huko ukingo wa magharibi. Duru za jeshi zinasema afisa huyo amesimamishwa kwa makosa aliyoyafanya kama kiongozi wa kikosi hicho, na atasubiri matokeo ya uchunguzi kabla kesi yake kuamuliwa.

Walioshudia maujai hayo wamesema wanajeshi wa Israel walifyatua risasi wakati waandamanaji walipoanza machafuko, kisa ambacho kimeelezewa kuwa tisho kubwa kwa mkataba wa kusitisha mapigano ulioafikiwa kati ya Israel na Palestina.