Jee Zanzibar ni dola ?
8 Julai 2008Matangazo
Mjadala mkubwa uliibuka jana katika kikao cha Baraza la Wawakilishi la Zanzibar baada ya wajumbe wa baraza hilo kuhoji inakuwaje baadhi ya watu kuanza kuchezea suala la Zanzibar kuwa sio nchi, hali inayotishia mustakbali mbaya katika muungano wa Zanzibar na Tanganyika ambao umedumu kwa miaka 44 sasa.
Salma Said ametutumia ripoti ifuatayo kutoka Zanzibar...