1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JEDDAH : Annan kuteuwa msuluhishi kwa Israel na Hizbollah

5 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDFA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amesema atamteuwa mjumbe wa siri kusuluhisha kati ya Israel na wapiganaji wa Hizbollah katika kusaidia kuachiliwa huru kwa wanajeshi wawili wa Israel wanaoshikiliwa na Hizbollah.

Msemaji wa Annan amesema pande zote mbili zimewasilisha maombi ya kutafuta suluhisho.Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Jeddah Saudi Arabia Annan amekataa kutaja jina la mjumbe huyo kwa kusema kwamba kwa kufanya hivyo mjumbe huyo ataweza kufanya kazi zake kwa hadhari.

Annan amekuwa katika ziara ya Mashariki ya Kati yenye lengo la kuimarisha kuungwa mkono kwa azimio la Umoja wa mataifa ambalo limekomesha mapigano kati ya Israel na Hizbollah.