1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Japan yashukisha kiwango cha tahadhari kuhusu tsunami

1 Januari 2024

Japan imeondoa tahadhari yake kubwa kuwahi kutolewa kuhusu matetemeko makubwa ya chini ya bahari kufuatia mfululizo wa matetemeko makubwa ya ardhi hii leo

https://p.dw.com/p/4am7S
Mianya ya ardhini kutokana na matetemeko makubwa ya ardhi nchini Japan, Januari 1, 2024
Mianya ya ardhini kutokana na matetemeko makubwa ya ardhi nchini JapanPicha: Kyodo News/AP/picture alliance

Tetemeko hilo kubwa la 7.6 kwenye kipimo cha Richter lilisababisha kuzuka kwa moto na kuporomoka kwa majengo katika maeneo ya Magharibi ya kisiwa chake kikubwa cha Honshu.

Haikubainika wazi idadi ya watu waliofariki ama kujeruhiwa.

Msemaji wa serikali Yoshimasa Hayashi, amesema takriban nyumba sita ziliharibiwa na matetemeko hayo huku watu kadhaa wakikwama ndani yake.

Soma pia:Tsunami yaipiga Japan

Moto pia ulizuka katika mji wa Wajima na takriban nyumba 30,000 kukosa huduma za umeme.

Awali Mamlaka ya Hali ya Hewa ilitoa tahadhari ya tetemeko kubwa la chini ya bahari katika eneo la Ishikawa na onyo lamatetemeko ya wastani kwa maeneo mengine ya Pwani ya Magharibi ya kisiwa cha Honchu pamoja na visiwa vya Hokkaido katika eneo la Kaskazini.

Masaa machache baadaye, Mamlaka hiyo ilishusha kiwango cha tahadhari hii ikimaanisha kuwa mawimbi huenda yakafikia hadi mita 3.