1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JAMAA ISLAMIYA NA AL QAEDA

6 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDOL

CAIRO:

makamo wa kiongozi wa mtandao wa Al Qaeda,Ayman al-Zawahiri ametangaza baadhi ya wakereketwa wa Jamaa Islamiya nchini Misri , wanajiunga na mtandao wa al qaeda ulimwenguni.Katika risala yake iliotangazwa na kituo cha Tv cha AL JAZEERA, mzaliwa huyo wa Misri Zawahiri aliwakaribisha viongozi kadhaa wa Jamaa Islamiya chini ya paa la al qaeda.Jamaa Islamiya ni kikundi kilichokuwa nyuma ya kuuliwa kwa rais Anwar sadat wa Misri, 1981 na kkaendelea kupambana na jeshi la Misri mnamo miaka ya 1980.Kampeni ya jamaa Islamiya nchini Misri ya muda wa miaka 6 mnamo miaka ya 1990ini ilisababisha vifo vya hadi watu 1,000 humo nchini.