1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 177 waokolewa kivukoni Italia

30 Septemba 2023

Walinzi katika eneo la pwani la Italia wamefanikiwa kuwaokoa watu 177 wakiwemo mabaharia 27 kutoka kwenye kivuko kilichoshika moto.

https://p.dw.com/p/4WzmN
Italien, Lampedusa | Migranten werden von Sanitätern versorgt
Picha: Cecilia Fabiano/ZUMA Press/picture alliance/AP

Walinzi katika eneo la pwani la Italia wamefanikiwa kuwaokoa watu 177 wakiwemo mabaharia 27 kutoka kwenye kivuko kilichoshika moto kilichokuwa kikiwavusha kutoka kisiwa cha Lampedusa nchini Italia kuelekea Porto Empedocle huko Sicily.Taarifa ya mamlaka yenye dhima ya ulinzi katika pwani hiyo ilisema miongoni mwa waliokuwemo katika kivuko hicho, ambacho moto ulizuka kutoka katika injini yake ni pamoja na wahamiaji 83 ambao walikuwa wakihamiashwa kutoka Lampedusa.Abiria wote walihamishiwa kwenye chombo cha walinzi wa pwani, na kwa sasa wako njiani kulekea Porto Empedocle, isipokuwa watatu ambao wamerejea Lampedusa.