1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Italia - Bolsonaro hajaomba uraia wa Italia

10 Januari 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Antonio Tajani amesema haamini iwapo rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro, anaweza kuomba uraia wa Italia na wala hajaomba.

https://p.dw.com/p/4LweM
Brasilien Brasilia 2019 | Jair Bolsonaro, Präsident & Edir Macado & Silvio Santos
Picha: Evaristo Sa/AFP/Getty Images

Vyombo vya habari vya Brazil vimeripoti kuwa baada ya wafuasi wa Bolsonaro kuyavamia majengo ya serikali mjini Brasilia siku ya Jumapili, rais huyo wa zamani alikuwa akitafuta uraia wa Italia.

Wakati huo huo, Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva ameahidi kuwawajibisha wote waliohusika na kuyavamia majengo hayo ya serikali. Polisi nchini Brazil hadi jana walikuwa wamewakamata wafuasi wapatao 1,500 kutokana na kulivamia bunge, mahakama kuu na makaazi ya rais.