1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaionya Hizbullah kuiingiza Lebanon vitani

22 Oktoba 2023

Jeshi la Israel limesema mashambulizi yanayofanywa na kundi la wanamgambo la Hizbullah yanahatarisha kutanuka kwa mzozo kati yake na wanamgambo wa Hamas na kuingia nchini Lebanon.

https://p.dw.com/p/4XryU
Moshi ukifuka kwenye mji wa Al-Marion nchini Lebanon baada ya kombora la Israel iliyodai kujibu mashambulizi ya kundi la Hizbullah siku ya tarehe 15 Oktoba 2023.
Moshi ukifuka kwenye mji wa Al-Marion nchini Lebanon baada ya kombora la Israel iliyodai kujibu mashambulizi ya kundi la Hizbullah siku ya tarehe 15 Oktoba 2023.Picha: Ali Hashisho/Xinhua/IMAGO

Msemaji wa jeshi la ulinzi la Israel, Jonathan Conricus, amesema kile Hizbullah inachokifanya, ni kuiingiza Lebanon vitani na hilo halitowafaidisha kwa namna yoyote.

Kupitia mmoja ya viongozi wake, Naim Qassem, kundi hilo limeonya kwamba litauingilia kikamilifu mgogoro huo iwapo litaona haja ya kufanya hivyo. 

Soma zaidi: Marekani yaitaka Hizbollah kuondoka Syria

Hizbullah ina mafungamano na kundi la Hamas, lililofanya mashambulizi ya Oktoba 7 kusini mwa Israel na kusababisha mauaji ya Waisraelii 1,400. 

Israel ilijibu kwa kuishambulia Gaza na kusababisha mauaji ya zaidi ya Wapalestina 4,000 hadi sasa.