Israel yaendeleza mashambulizi yake Gaza na Lebanon
9 Novemba 2024Jeshi hilo limesema limelenga maeneo ya mawasiliano na ya kutengeneza silaha ya kundi hilo pamoja na miundombinu yao mjini Dahiyeh.
Jeshi limesisitiza kuwa kabla ya operesheni hiyo kuanza, hatua kadhaa zilichukuliwa ili kuepuka kuwashambulia raia.
70% ya waliouawa ukanda wa Gaza ni wanawake na watoto
Katika taarifa ya jeshi hilo iliyotumwa katika mtandao wa Telegram, shambulizi jengine lililofanywa na jeshi la ardhini limewauwa wanamgambo kadhaa katika kambi ya Jabalia kaskazini mwa Gaza.
Israel ilianzisha kampeni yake dhidi ya kundi la Hamas Oktoba 7 mwaka 2023 baada ya kundi hilo kushambulia kusini mwa Israel na kusababisha vifo vya watu 1,200. Tangu Israel ianze mashambulizi hayo, Wapalestina zaidi ya 40,000 wameuwawa huku mamilioni kadhaa wakipoteza makaazi yao.