1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaendelea kuishambulia Lebanon

4 Oktoba 2024

Israel imefanya mashambulizi makali usiku wa kuamkia leo kwenye viunga vya mji mkuu wa Lebanon, Beirut katika wakati mzozo wa karibu mwaka mmoja kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Hezbollah ukitanuka.

https://p.dw.com/p/4lPJw
Israel Lebanon
Vifaru vya Israel kwenye mpaka wa nchi hiyo na Lebanon.Picha: Jalaa Marey/AFP/Getty Images

Milipuko mikubwa ya makombora yaliyofyetuliwa na ndege za kivita za Israel iliutikisa mji huo na moto mkubwa pamoja na wingu zito la moshi vilionekana kwenye anga ya Beirut hadi mapema alfajiri. 

Shirika la habari la Lebanon limeripoti kwamba kwa jumla kulikuwa na mashambulizi yanayopindukia 10, likiwemo moja lililosababisha kufungwa kwa barabara muhimu inayoziunganisha Lebanon na Syria. 

Soma zaidi: Israel yasema wanamgambo 15 wameuwawa Lebanon

Njia karibu na mpaka wenye shughuli nyingi wa Masnaa inatumiwa na makumi kwa maelfu ya watu wanaokimbia vita nchini Lebanon.

Israel haikusema chochote kuhusu mashambulizi hayo ya usiku kucha na hadi sasa bado hakuna takwimu rasmi za vifo au majeruhi kutokana na hujuma hizo.