1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Waathiriwa wa tetemeko la ardhi kusaidiwa na India

23 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEPF

Pakistan imelikubali pendekezo la India kufungua vituo vya kutoa misaada katika eneo la Kashmir linalodhibitiwa na India.Katika vituo hivyo, waathiriwa wa tetemeko la ardhi kutoka Pakistan,wataweza kupokea matibabu.Kwa mujibu wa India,katika vituo hivyo vinavyotazamiwa kuanza kufanya kazi siku ya Jumanne,kutatolewa pia misaada ya chakula,maji ya kunywa na mavazi.Kwa upande mwingine Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia zaidi.Mjumbe wa Umoja huo amesema bado vijiji mia kadhaa nchini Pakistan vinangojea kupokea msaada kwa sababu ya matatizo ya usafiri.Kuna khofu kuwa hadi watu 80,000 wamefariki katika tetemeko la ardhi lililotokea tarehe 8 Oktoba.