1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Pakistana na India zajadili kuruhusu watu wa Kashmir.

19 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEQS

Nchi za Pakistan na India zimekuwa katika majadiliano ya namna ya kuwasaidia watu waliokumbwa na dhahama ya tetemeko la ardhi katika eneo la Kashmir,kwa kuwaruhusu watu kuvuka mpaka unaogawanya jimbo lenye ugomvi baina ya pande hizo mbili.

Maelfu ya watu walionusurika na tetemeko hilo la ardhi lililotokea tarehe 8 mwezi huu,bado wanahitaji kwa kiasi kikubwa msaada.

Halikadhalika matetemeko madogomadogo yanayotokea mara kwa mara yanazidisha ukali wa maisha kwa watu walionusurika na tetemeko lile kubwa.

Kiasi cha watu 54,000 wanahofiwa wamekufa wakati tetemeko la ardhi lilipopiga siku 11 zilizopita na pia kusababisha watu milioni 2.5 kukosa makazi.