1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Mtuhumiwa wa al Qaeda atajwa kwa jina

12 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDMI

Pakistan imetaja jina la raia wa Kingereza anaesemekana kuwa ni mtu muhimu kuhusika na madai ya Uingereza ya kuwepo njama ya kutaka kuripua ndege zinazokwenda Marekani kupitia bahari ya Atlantik.Wizara ya mambo ya kigeni ya Pakistan imesema,Rashid Rauf anaeshukiwa kuwa na uhusiano na al Qaeda,na akiwa mmoja kati ya watu kadhaa waliokamatwa hivi karibuni nchini Pakistan aliwasiliana na watayarishaji wa njama ya mashambulio hayo.Askari polisi nchini Uingereza wamewakamata washukiwa 24,katika miji ya London na Birmingham,wengi wao ni Waislamu.Benki Kuu ya Uingereza imezuia akaunti za washukiwa 19. Wachunguzi wanaamini washukiwa hao walipanga kuchukua miripuko ya maji maji ndani ya ndege katika mikoba yao na baadae walidhamiria kuyatengeneza mabomu hayo.