1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iraq yajitolea kusimamia juhudi za kumaliza vita Yemen

Sylvia Mwehozi
23 Julai 2023

Iraq imejitolea kuwa msuluhishi wa pande zinazozozana nchini Yemen, katika juhudi za kumaliza vita vya muda mrefu. Maelfu ya watu wamekufa kutokana na mzozo wa Yemen.

https://p.dw.com/p/4UHmt
Yemen Sanaa
Wafungwa wa Yemen walioachiliwa wakiwasili mjini SanaaPicha: KHALED ABDULLAH/REUTERS

Iraq imejitolea kuwa msuluhishi wa pande zinazozozana nchini Yemen, katika juhudi za kumaliza vita vya muda mrefu. Waziri wa mambo ya kigeni wa Iraq Fouad Hussein ametoa pendekezo hilo, wakati wa ziara ya waziri wa masuala ya kigeni wa Yemen Ahmed bin Mubarak.Wasaudia wakutana na waasi wa Houthi kutafuta amani Yemen

Waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iraq, waliudhibiti mji mkuu Sanaa mwaka 2014, kabla ya muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudia kuingilia kati kuisaidia serikali inayoungwa mkono kimataifa. Kwa sasa mapambano bado yamesitishwa licha ya makubaliano ya kuweka silaha chini kati ya pande zinazozozana yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa kumaliza muda wake tangu mwezi Oktoba mwaka jana.

Maelfu ya watu wamekufa kutokana na mzozo wa Yemen katika kile Umoja wa Mataifa unachokiita kuwa mgogoro mbaya zaidi wa kiutu kuwahi kutokea duniani.