1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yakanusha kuwasaidia waasi wa Houthi

20 Novemba 2023

Iran yakanusha madai ya Israel ya kuwasaidia waasi wa houthi kuiteka meli ya mfanyabiashara wa Tel Aviv

https://p.dw.com/p/4ZArU
Rais wa Iran Ebrahim Rais akiwa katika mahojiano na mwandishi wa habari
Rais wa Iran Ebrahim Rais akiwa katika mahojiano na mwandishi wa habariPicha: Iranian Presidency/Zuma/picture alliance


Iran imepuzilia mbali madai ya Israel iliyoyaita batili kwamba waasi wa Houthi wanafanya kazi kwa ushirikiano na serikali ya Iran wakati walipoiteka meli inayomilikiwa na ya mfanyabiashara mmoja wa Israel katika bahari ya Shamu. 

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nchi za nje wa Iran Nasser Kanani, amesema waasi wa Houthi wanawakilisha mataifa yao na wanachukua hatua kwaajili ya manufaa ya mataifa yao.

Ameongeza kuwa utawala wa Israel hautaki kukubali umepata pigo kubwa katika vita vyake dhidi ya Palestina na unatafuta sababu za kuhalalisha kushindwa kwake  kwa kuishutumu Iran. 

Soma pia:Ujerumani yapekua nyumba zinazohusishwa na harakati za Iran

Waasi wa Houthi waliiteka meli hiyo ya Galaxy Leader jana Jumapili, siku chache baada ya kutishia kulenga meli za Israel katika bahari hiyo kufuatia vita inavyoviendeleza dhidi ya kundi la wanamgambo la Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Kulingana na taarifa ya ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, meli hiyo ilitekwa na waasi wa Houthi kupitia muongozo uliotolewa na  Iran.