1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yafanya mazishi ya muasisi wa programu ya nyuklia

Angela Mdungu
30 Novemba 2020

Iran imefanya ibada ya maziko ya aliyekuwa mwanasayansi Mohsen Fakhrizadeh aliyeanzisha program ya nyuklia ya taifa hilo miongo miwili iliyopita. Waziri wa ulinzi aapa kuiendeleza kazi ya mwanasanyansi huyo

https://p.dw.com/p/3m1YG
Iran Teheran | Beisetzung des getöteten iranischen Atomforschers Mohsen Fachrisadeh
Picha: Iranian Defense Ministry/AP PHoto/picture alliance

Jeshi maalumu la heshima, leo lilibeba jeneza la mwili wa mwanasayansi Mohsen Fakhrizadeh aliyeripotiwa kuuawa kwa mbinu ya kijeshi ya kushtukiza Ijumaa iliyopita. Maafisa wa Iran wanaituhumu Iran kuwa ndiyo iliyohusika na shambulio hilo. 

Mwanasayansi huyo aliyeuawa alikuwa mkuu wa program ya AMAD, ambayo Israeli na mataifa ya Magharibi yamekuwa yakiituhumu kuwa ni operesheni ya kijeshi inayofanya upembuzi yakinifu ili kutengeneza silaha za nyuklia.

Mohsen Fakhrizadeh |  iranischer Atomwissenschaftler
Mohsen Fakhrizadeh alishambuliwa na kuuawa TehranPicha: IRNA

Miongoni mwa waliohudhuria ibada ya maziko ya Mohsen Fakhrizadeh ni pamoja na waziri wa ulinzi, Amir Hatami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la walinzi wa mapinduzi ya Iran Jenerali Hossein Salami, mkuu wa mpango wa nyuklia wa kiraia Ali Akbar Sahei waziri wa Intelijensia  Mamoud Alavi. Katika shughuli hiyo waziri wa ulinzi wa Iran Amir Hatami alizikosoa nchi ambazo hadi sasa hazijalaani mauaji ya Fakhrizadeh huku waziri wa ulinzi akiapa kuwa Iran italipiza kisasi kwa mauaji hayo. "Na maadui wanapaswa kufahamu kuwa, wameshindwa kwa mara ya kwanza. Kama walidhamiria kumuua shujaa wetu ili jina lake lipotee, sasa jina lake linaimwa kila mahali na amekuwa mfano kwa wote wanaoianza safari ya mapambano.

Soma zaidi: Israel yanyooshewa kidole mauaji ya mwanasayansi wa Iran

Iran yaapa kulipiza kisasi 

Kwa mujibu wa televisheni ya taifa ya Iran, ikivinukuu vyanzo mbalimbali bila kutaja majina, inasema silaha iliyopatikana kwenye eneo yalikotokea mauaji hayo inaonekana kuwa ya Israel. Hata hivyo Israeli, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikituhumiwa kuwauwa wanasayansi wa nyuklia kwa zaidi ya muongo mmoja imekataa mara kadhaa kulizungumzia shambulio hilo.

Iran Anschlag gegen Mohsen Fakhrizadeh
Gari alimokuwa Mohsen FakhrizadehPicha: IRIB NEWS AGENCY/AFP

Israel inasisitiza kuwa Iran inaendelea na shauku yake kubwa ya kuzalisha silaha za nyuklia, ikinyooshea kidole mradi wa silaha za makombora na utafiti wa teknolojia nyingine za silaha. Kwa upande wake Iran iimekuwa ikidai kwa muda mrefu kuwa, mpango wake wa nyuklia ni wa amani.

Miongoni mwa waliohudhuria ibada ya maziko ya Mohsen Fakhrizadeh ni pamoja na waziri wa ulinzi, Amir Hatami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la walinzi wa mapinduzi ya Iran Jenerali Hossein Salami, mkuu wa mpango wa nyuklia wa kiraia Ali Akbar Sahei waziri wa Intelijensia  Mamoud Alavi. Katika shughuli hiyo waziri wa ulinzi wa Iran Amir Hatami alizikosoa nchi ambazo hadi sasa hazijalaani mauaji ya Fakhrizadeh huku waziri wa ulinzi akiapa kuwa Iran italipiza kisasi kwa mauaji hayo.

Umoja wa Falme za kiarabu, ambayo hivi karibuni iliingia kwenye makubaliano ya kurejesha mahusiano ya kidiplomasia ilitoa kauli ya kuyalaani mauaji hayo ikisisitiza kuwa huenda yakachochea mtafaruku zaidi kwenye ukanda huo. Nayo Jordan, mshirika mwaminifu wa Marekani, imelaani mauaji ya mwanasayansi huyo wa Iran ikitaka juhudi za pamoja za kuepuka migogoro katika eneo la mashariki ya kati.

afp, reuters, ap, dpa