1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaIran

Iran yaapa kulipa kisasi kwa shambulio la bomu huko Kerman

5 Januari 2024

Rais wa Iran Ibrahim Raisi na Kamanda Mkuu wa jeshi la walinzi wa mapinduzi Hossein Salami wameapa kulipiza kisasi kufuatia shambulio la bomu wakati wa kumbukumbu ya miaka minne ya mauaji ya jenerali Qasem Suleiman.

https://p.dw.com/p/4at26
Iran Kerman 2024 | ahari za mlipuko wa bomu
Shambulio wakati wa kumbukumbu ya kifo cha Qassim Soleimani lilisababisha vifo na uharibifu wa mali.Picha: Fars/ZUMA Press Wire via picture alliance

Kamanda huyo mkuu wa jeshi la walinzi wa mapinduzi ameeleza kuwa, watawasaka wote waliohusika na shambulio hilo.

Katika hotuba iliyopeperushwa kwenye runinga ya taifa, Rais Ibrahim Raisi amesema dunia nzima inajua uwezo wa nchi yake na kwamba vikosi vyao vitachukua hatua katika wakati sahihi.

Takriban watu 100 waliuawa katika mji wa Kerman wakati wa hafla ya kumuenzi kamanda Qassem Soleiman aliyeuawa mwaka 2020 nchini Iraq.

Kundi linalojiita Dola la Kiislamu limedai kuhusika na shambulio hilo na kwamba wapiganaji wake wawili waliripua mabomu mbele ya umati uliokusanyika karibu na kaburi la Qassem Soleiman.