1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yaahidi kuishambulia tena Israel endapo itashambuliwa

4 Oktoba 2024

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iran, Abbas Araghchi, amesema leo kwamba Tehran itajibu vikali iwapo Israel itaamua kulipa kisasi kwa mashambulizi ya makombora yaliyofanywa Iran dhidi ya nchi hiyo mnamo Oktoba Mosi.

https://p.dw.com/p/4lQPy
Abbas Araghchi
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iran, Abbas AraghchiPicha: Frank Franklin II/AP Photo//picture alliance

Araghchi aliyatoa matamshi hayo akiwa ziarani nchini Lebanon kwa mazungumzo na maafisa wa nchi hiyo inayoshuhudia makabiliano kati ya vikosi vya Israel na wanamgambo wa Hizbullah. 

Mwadiplomasia huyo wa ngazi za juu wa Iran alisema pindi Israel itaamua kuchukua hatua ya kulipa kisasi, Tehran nayo itajibu kwa kuishambulia miundombinu ya mafuta na gesi ya Israel. 

Soma zaidi: Uchambuzi: Mambo gani yamo kwenye mkakati wa Iran, Israel?

Kauli ya Araghchi yanakuja siku moja tu baada ya Rais Joe Biden wa Marekani kuashiria kwamba Israel ina mipango ya kuilenga miundombinu ya mafuta ya Iran kama jibu kwa mashambulizi ya makombora ya masafa yaliyovurumishwa na dola hiyo ya Uajemi mwanzoni mwa wiki hii.