1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran : Wabunge waidhinisha adhabu kali dhidi ya wanawake

20 Septemba 2023

Wabunge wa Iran wamepitisha muswada wa kutaka adhabu kali zaidi kwa wanawake wanaokiuka kanuni ya mavazi ya Kiislamu.

https://p.dw.com/p/4WaWH
Wanawake nchini Iran wamekuwa wakikaidi kanuni kali za mavazi ya Kiislamu nchini humo zinazowataka kufunika vichwa na mavazi ya staha.
Wanawake nchini Iran wamekuwa wakikaidi kanuni kali za mavazi ya Kiislamu nchini humo zinazowataka kufunika vichwa na mavazi ya staha.Picha: UGC

Kulingana na vyombo vya habari vya serikali, adhabu hizo ni pamoja na kifungo cha hadi miaka 10.

Bunge la Iran limeidhinisha  kile ilichokiita "Uungaji  mkono tamaduni ya uvaaji  Hijab na unadhifu" utakaofanyiwa majaribio kwa miaka mitatu, limeripoti shirika la habari la IRNA.

Hata hivyo muswada huo bado unatakiwa kuidhinishwa na Baraza la uongozi, lenye nguvu na ushawishi mkubwa katika Jamhuri hiyo ya Kiislamu, maarufu "Guardian Council".

Tangu mwaka uliopita, wanawake nchini Iran wamekuwa wakikaidi kanuni kali za mavazi ya Kiislamu nchini humo zinazowataka kufunika vichwa na mavazi ya staha, na hasa baada ya maandamano makubwa kufuatia kifo cha Mahsa Amini mikononi mwa polisi jamii.

Soma pia:

Wairan wakumbuka mwaka mmoja tangu kifo cha Mahsa Amini