1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran haitoishambulia Israel iwapo usitishwaji vita utafikiwa

13 Agosti 2024

Maafisa 3 waandamizi wa Iran wanasema makubaliano ya kusitisha vita vya Gaza kutokana na mazungumzo yanayotarajiwa kufanyika wiki hii, ndilo jambo la pekee litakaloipelekea Iran kutofanya mashambulizi ya kulipiza kisasi.

https://p.dw.com/p/4jQbR
Iran | Ismail Haniyeh | Tehran
Ismail Haniyeh kiongozi wa kundi la Hamas anaedaiwa kuuwawa na Israel nchini IranPicha: Rouzbeh Fouladi/ZUMAPRESS.com/picture alliance

Iran inataka kulipiza kisasi dhidi ya Israel, kufuatia mauaji ya kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh.

Mmoja wa maafisa hao wa Iran ambaye ni afisa mwandamizi wa usalama amesema Iran pamoja na washirika wake kama Hezbollah watashambulia iwapo mazungumzo ya Gaza hayatopata mwafaka au iwapo Israel itakuwa inajikokota katika suala la upatikanaji wa suluhu.

Shambulizi la Israel laua watu 10 wa familia moja Gaza

Haya yanafanyika wakati ambapo Cyprus imekamilisha maandalizi ya kuwaondoa raia wake nchini Lebanon na Israel.

Haya yamethibitishwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Cyprus, Constantinos Kombos. Mpango unakuja wakati ambapo kuna hofu ya Iran na washirika wake kufanya mashambulizi makubwa hivi karibuni na kuvitanua vita hivyo vya Mashariki ya Kati.