1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Irak yalaani mashambulizi ya angani ya Marekani Baghdad

22 Novemba 2023

Serikali ya Iraq imelaani mashambulizi ya angani ya usiku kucha yaliyofanywa na Marekani kusini mwa Baghdad na kusababisha vifo vya wanachama 8 wa kundi la Kataib Hezbollah, linaloungwa mkono na Iran.

https://p.dw.com/p/4ZKRi
Wanajeshi wa Marekani wakiwa katika gwaride la kijeshi Iraq
Wanajeshi wa Marekani wakiwa katika gwaride la kijeshi IraqPicha: Jewel Samad/AFP/Getty Images

Katika taarifa, kundi hilo lililojihami limesema mashambulizi hayo yamewauwa hao wanachama wake katika ngome yake ya Jurf al-Sakhar. Kataib Hezbollah limetishia kufanya mashambulizi zaidi iwapo Marekani itaendelea kushambulia.

Marekani imefanya msururu wa mashambulizimawili Iraq tangu jana na hiyo kutokana na zaidi ya mashambulizi 60 yaliyofanywa na wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran dhidi ya majeshi katika eneo hilo.

Soma pia:Marekani imesema tayari imeshambuliwa karibu mara 66 na wanamgambo nchini Iraq

Hadi wiki hii, Marekani ilikuwa haijafanya uamuzi wa kulipiza kisasi nchini Iraq kwasababu ya hali tete ya kisiasa nchini humo, ambapo marekani inatafuta ushirikiano wa karibu na pia ilikuwa haitaki ionekane kana kwamba ni kutanuka kwa vita vya Israel dhidi ya hamas katika eneo hilo la Mashariki ya Kati.