1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji Tunisia waelezea utayari wa kurudi makwao

28 Juni 2024

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesema wahamiaji wengi nchini Tunisia wameeleza utayari wao wa kurudishwa makwao katikati ya ongezeko la chuki na shinikizo la mataifa ya Ulaya kuzuia wimbi la uhamiaji.

https://p.dw.com/p/4heMa
Wahamiaji -Tunisia
Wahamiaji wa kiafrika nchini TunisiaPicha: Hazem Turkia/AA/picture alliance

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesema wahamiaji wengi nchini Tunisia wameeleza utayari wao wa kurudishwa makwao katikati ya ongezeko la chuki na shinikizo la mataifa ya Ulaya kuzuia wimbi la uhamiaji.

Msemaji wa shirika hilo ameliambia shirika la habari la AFP kuwa, kati ya Januari mosi na Juni 25, IOM iliwezesha kurejeshwa kwa hiari watu 3,500 kutoka Tunisia hadi katika nchi zao za asili.Zaidi ya watu 63,000 wamepotea au kutoweka kwa uhamiaji. Zaidi ya watu 63,000 wamepotea au kutoweka kwa uhamiaji

Mpango wa IOM wa kuwarudisha kwa hiari wahamiaji, ikiwemo kutoa safari za ndege bila malipo, umeshuhudia ongezeko la asilimia 200 ya wahamiaji waliojiandikisha ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2023.

Wahamiaji ambao wengi wao wanatokea Gambia, Burkina Faso na Guinea waliingia nchini Tunisia kwa matumaini ya kuvuka na kuingia Ulaya.