1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoIndonesia

Indonesia yawashtaki waliosababisha vifo vya watu 135

16 Januari 2023

Mahakama moja ya Indonesia imeanza kusikiliza kesi dhidi ya watu watano wanaoshtakiwa kwa tuhuma za uzembe uliosababisha vifo vya watu 135 vilivyotokea katika uwanja wa mchezo wa soka

https://p.dw.com/p/4MEbk
Indonesien | Joko Widodo
Picha: Tatan Syuflana/AP Photo/picture alliance

Polisi walifyetua gesi ya kutowa machozi ndani ya uwanja huo baada ya mashabiki kufurika uwanjani kufuatia kushindwa kwa  timu ya Arema FC na mpinzani wake Persebaya Surabaya katika mechi ya nyumbani kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 23. Hatua hiyo ilisababisha tukio baya kabisa katika historia ya michezo duniani la mkanyagano mnamo mwezi Oktoba mosi mwaka jana. Rais wa nchi hiyo Joko Widodo aliunda tume ya uchunguzi wa tukio hilo ambayo imetoa tathmini yake kwamba gesi ya kutowa machozi ndio chanzo kilichosababisha msongamano wa mashabiki.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW