1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Indonesia yazungumzia ushirikiano wa China amani ya Myanmar

22 Februari 2023

Indonesia imesema inauthamini uungaji mkono wa China kwa makubaliano ya amani ya Jumuiya ya Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia, ASEAN, kwa ajili ya kuhitimisha utawala wa kiimla wa kijeshi nchini Myanmar.

https://p.dw.com/p/4NpVQ
Indonesien | ASEAN Gipfel 2023 in Jakarta
Picha: Achmad Ibrahim/AP Photo/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia, Retno Marsudi, amesema anauthamini uungaji mkono wa China wenye kuzingatia mambo matano muhumu kwa ajili ya kuhitimisha utawala wa kiimla wa kijeshi nchini Myanmar.

Retno ameyazungumza hayo baada ya mkutano wake na mwenzake wa China, Qin Gang mjini Jakarta.

Myamnar imeingia katika mfululizo wa vurugu, kudorora kwa uchumi pamoja na ukosefu wa utulivu wa kisiasa tangu mapema 2021.

Mataifa yaliyo katika muungano wa ASEAN, ambayo Indonesia wakati huu inashikilia uwenyekiti wa kupokezana, yanakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na watawala wa kijeshi kutokuwa tayari kutekeleza makubaliano yaliyoridhiwa muda mfupi baada ya mapinduzi ya Februari mwaka 2021, ambayo yalisainiwa na kiongozi mkuu wa kijeshi.