1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

India:Tumekamilisha oparesheni ya uokoaji mkasa wa treni

Hawa Bihoga
4 Juni 2023

Mamlaka nchini India zimekamilisha operesheni za uokoaji kufuatia ajali mbaya ya treni nchini humo, ambapo hitilafu za mifumo ya mawasiliano zimetajwa chanzo cha ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu wasiopungua 275.

https://p.dw.com/p/4SBBs
Indien Odisha Balasore | Zugunglück
Picha: ADNAN ABIDI/REUTERS

Katibu kiongozi wa jimbo la mashariki la Odisha Pradeep Jena, amesema idadi ya vifo kutokana na ajali hiyo iliyotokea Ijumaa imerekebishwa kutoka 288, baada ya kubainika kuwa baadhi ya maiti zilikuwa zimehisabiwa mara mbili.

Amewaambia waandishi wa habari kuwaidadi hiyo haina uwezekano wa kuongezeka baada ya kukamilika kwa operesheni hiyo.

Karibu watu 1,200 walijeruhiwa wakati treni ya abiria ilipogonga nyingine ya mizigo iliyokuwa imesimama, kuacha njia na kugonga treni nyingine ya abiria iliyokuwa inapita katika upande mwingine karibu na wilaya ya Balasore.

Soma pia:Hakuna manusura wengine wa ajali ya treni India

Zaidi ya watu 900 wameruhusiwa kutoka hospitali wakati 260 walikuwa wanaendelea kutibiwa, huku mgonjwa mmoja akiwa hali mahututi.