IEBC na Safaricom zatoa vielelezo kwa CORD
13 Machi 2013Matangazo
Wakati huo huo Mrengo wa Jubilee unaoongozwa Rais Mteule Uhuru Kenyatta nao pia umetaka kukabidhiwa takwimu hizo.
Mawakili wa mrengo wa CORD waliwasilisha ombi hilo mahakamani baada ya Tume ya IEBC kukataa kuwapa nakala za fomu za matokeo ya urais ili waweze kuwasilisha kesi ya kupinga kutangazwa kwa Uhuru Kenyatta kama mshindi wakidai uchaguzi ulikumbwa na hitilafu nyingi. Sikiliza taarifa ya Alfred Kiti kutoka Kenya kwa kubonyeza alama ya masikioni hapo chini.
Mwandishi Alfred Kiti
Mhariri Mohammed Khelef