1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IDF yawaamuru Wapalestina kuhama tena eneo salaama

22 Julai 2024

Jeshi la Israel limetoa amri mpya ya kuwataka Wapalestina waondoke katika sehemu moja ya Ukanda wa Gaza iliyokuwa imetengwa kwa shughuli za kibinadamu.

https://p.dw.com/p/4ibbr
Ukanda wa Gaza | Wapalestina wakihama
Wapalestina wanahama kutoka eneo la Kan Younis lenye mashambulizi makali ya Israel Picha: Mohammed Salem/REUTERS

Mamia ya Wapalestina waliotaharuki wameanza kulikimbia eneo hilo la Al Mawasi lilioko kati ya miji ya Khan Yunis na Rafah.

Jeshi la Israel leo limetangaza kwamba linapanga kuanza operesheni maalum dhidi ya wanamgambo wa Hamas waliojikusanya kwenye eneo hilo na kulitumia kufyetuwa maroketi kuelekea Israel.

Soma pia:Mkuu wa haki UN asema viwango vya vita vimekiukwa kikatili Gaza

Eneo linalotajwa na Israel linahusisha sehemu ya mashariki ya mji wa Mawasi ambako ni eneo lililotengwa kwa shughuli za msaada, lililoko Kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Tangazo la Israel limekuja katika wakati ambapo maafisa wa Marekani na Israel wameelezea matumaini yao ya kukaribia kufikiwa makubaliano katika mazungumzo tete ya kutafuta usitishaji mapigano.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW