1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUturuki

Idadi ya vifo Uturuki na Syria yapindukia 20,000

10 Februari 2023

Waokoaji wamefanikiwa kuwapata manusura wengine kutoka kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka baada ya kutokea tetemeko kubwa la ardhi nchini Uturuki na Syria.

https://p.dw.com/p/4NJoK
Erdbeben Syrien Aleppo Rettungskräfte aus Iran
Picha: AFP

Binti mwenye umri wa miaka 10 aliokolewa usiku wa kuamkia leo kwenye wilaya Antakya siku tatu tangu janga hilo la asili lililopozipiga nchi hizo mbili na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 20,000.

Watu wengine kadhaa wamepatikana wakiwa hai katika majimbo ya Adiyaman na Kahramanmaras.

Hata hivyo vikosi vya uokozi vimesema matumaini ya kuwapata watu wengine zaidi wakiwa hai yanapungua.

Vifo vilivyosababishwa na tetemeko hilo la ardhi ambalo linatajwa kuwa baya zaidi katika kipindi cha muongo mmoja vimepindukia idadi ya wale waliopoteza maisha katika tetemeko lililoipiga Japan mwaka 2011.