1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya vifo kutokana na moto wa nyika Hawaii yafikia 100

15 Agosti 2023

Idadi ya watu waliokufa kutokana na janga la moto wa nyika uliokikumba kisiwa cha Maui kilicho sehemu ya jimbo la Hawaii nchini Marekani imefikia 100

https://p.dw.com/p/4VBGK
USA Lahaina | Gouverneur Josh Green nach Waldbränden auf Maui
Picha: Rick Bowmer/AP Photo/picture alliance

Mkasa huo unaotajwa kuwa ndiyo janga baya zaidi la moto nchini Marekani katika kipindi cha karne moja umeuteketeza kabisa mji wa kihistoria wa Lahaina.

Soma pia: Maafisa wa Hawaii wazuia watalii kwenda kisiwa cha Maui

Gavana wa jimbo la Hawaii Josh Green amesema kazi ya kuwatafuta waliopotea itachukua muda akikadiria kuwa miili ya watu 10 hadi 20 inawezaka kupatikana kila siku katika operesheni hiyo ambayo huenda itachukua alau siku 10 kukamilika.

Hadi sasa idadi ya watu waliopotea imefikia 1,300 na vikosi kadhaa vya watafutaji wanaosaidiwa na mbwa wa kunusa vimetawanywa katika maeneo yote ya kisiwa cha Maui. Mamlaka zimesema moto huo uliozuka wiki iliyopita kwa sehemu kubwa umedhibitiwa.