1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ICC yatoa waranti ya kukamatwa Netanyahu na maafisa wa Hamas

21 Novemba 2024

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC imetoa waranti wa kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, waziri wake wa zamani wa ulinzi Yoav Gallant pamoja na kiongozi wa kundi la Hamas Ibrahim Al-Masri.

https://p.dw.com/p/4nGAr
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu (katikati)Picha: Israel's Government Press Office/XinHua/picture alliance

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC imetoa waranti wa kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, waziri wake wa zamani wa ulinzi Yoav Gallant pamoja na kiongozi wa kundi la Hamas Ibrahim Al-Masri, ikiwashtumu kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, kuhusiana na vita katika Ukanda wa Gaza, na mashambulizi ya Oktoba 2023 yaliochochea mashambulizi ya Israel katika eneo hilo la Wapalestina. ICC yaanza kuchunguza uhalifu katika maeneo ya Wapalestina

Uamuzi huo unamfanya Netanyahu na wengine kuwa washukiwa wanaotafutwa kimataifa na kuna uwezekano wa kuwatenga zaidi na kufanya juhudi za majadiliano ya kumaliza vita kuwa ngumu zaidi. Netanyahu na viongozi wengine wa Israel walikosoa ombi la mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Karim Khan la waranti wa kukamatwa kwake na kulitaja kuwa chuki dhidi ya Wayahudi.

Rais wa Marekani Joe Biden pia alimkosoa mwendesha mashtaka huyo na kueleza kuunga mkono haki ya Israel kujilinda dhidi ya Hamas. Hamas pia ililaani ombi hilo.