HRW yaitolea wito Marekani kukomesha mauaji Darfur
5 Agosti 2023Matangazo
Wito huo umetolewa kwa Marekani wakati ikichukua urais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi Agosti.
Mkurugenzi mtendaji wa Human Rights Watch Tirana Hassan, amesema ulimwengu haupaswi kukaa kimya wakati miji katika mkoa wa Darfur ikiendelea kuteketea na kusababisha maelfu ya raia kukimbia.
Soma zaidi:Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa latoa wito wa kusimamisha mapigano nchini Sudan
Amesema serikali ya Marekani inapaswa kushinikiza ili kuhakikisha Baraza la usalama linachukua hatua za kuwalinda raia pamoja na kuwawajibisha wahusika wa mauaji.
Kiongozi wa kijeshi wa Sudan Abdel Fathah al-Burhan anapambana na makamu wake wa zamani Mohamed Hamdan Dagalo anayeongoza kikosi cha wanamgambo wa RSF tangu katikati ya mwezi wa nne.