1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HRW: Kenya ichunguze mauaji ya waandamanaji

Isaac Gamba21 Juni 2016

Shirika la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch limesema watu watano waliuliwa na wengine 60 kujeruhiwa na polisi katika mandamano ya CORD mkoa wa Nyanza. Otsieno Namwaya wa HRW azungumza na DW.

https://p.dw.com/p/1JAV5
Polisi akikabili waandamanaji Kenya
Picha: Reuters/T. Mukoya

[No title]

Human Rights Watch imetoa ripoti yake ya utafiti inayolituhumu jeshi la polisi nchini Kenya kutumia nguvu ya ziada kuwatawanya waandamanaji katika mkoa wa Nyanza magharibi mwa nchini hiyo mnamo Mei 23 na Juni 6 2016 ambapo watu watano waliuawa na wengine 60 kujeruhiwa. Maandamano hayo yaliitishwa na muungano wa upinzani nchini Kenya, CORD, unaotaka kuvunjwa kwa Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi ya nchi hiyo, IEBC. Isaac Gamba amezungumza na Otsieno Namwaya ambaye ni mtafiti wa shirika hilo kanda ya Afrika kutaka kujua walichobaini katika utafiti huo.