1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hospitali kuu ya al-Fashir Sudan yafungwa baada ya shambulio

10 Juni 2024

Hospitali kuu ya mji wa al-Fashir huko Sudan imeshambuliwa na kuifanya isiweze kutoa huduma. Taarifa hiyo imetolewa jana Jumapili na Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF), ambalo linasaidia kituo hicho.

https://p.dw.com/p/4gqp6
Sudan Al-Fashir | Moto sokoni baada ya mashambulizi ya RSF
Mwanamume akiwa amesimama huku moto ukiwaka katika eneo la soko la mifugo huko al-Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini mwa Sudan, Septemba 1, 2023.Picha: AFP

Wahudumu wa kujitolea katika maeneo hayo wanalinyooshea kidole kundi la wanamgambo wa RSF kutokana na shambulizi hilo.

Wapiganaji wa RSF ambao wameudhibiti mji mkuu wa Khartoum na maeneo mengi ya magharibi mwa Sudan pia wanataka kusonga mbele zaidi huku Umoja wa Mataifa ukisema raia wa Sudan wapo katika kitisho cha njaa.

Mji  wa al-Fashir ambao upo katika jimbo la Darfur upande wa kaskazini-magharibi mwa Sudan una jumla ya wakazi milioni 1.8 wakijumuishwa na watu waliokimbia makazi yao.

Kwa sasa mji huo umekuwa eneo la mapambano kati ya wanamgambo hao wa RSF na Jeshi la Sudan katika vita vilivyoanza Aprili 2023.