1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hofu ya uwekezaji Afrika

Admin.WagnerD23 Aprili 2013

Kongamano la Biashara la Afrika leo hii linaingia siku ya tatu, mjini Frankfurt, hapa Ujerumani ambapo wafanyabiashara zaidi ya 100 kutoka katika maeneo tofauti ya Afrika na Ujerumani wanakutana.

https://p.dw.com/p/18LUr
Public at the opening session of the German-African Energy Forum 2012; Hotel Grand Elysee (Hamburg), 23.04.2012; Copyright: DW/C. Vieira
Kongamani la nishati la Afrika na UjerumaniPicha: DW/C. Vieira

Katika kongamano hilo pamoja na mambo mengine imebainika kuwa wawekezaji wengi wa Ujerumani wenye nia ya kuwekeza Afrika, wanalitazama bara hilo kuwa ni eneo la hatari katika sekta ya uwekezaji ingawa washiriki wenyewe kutoka Afrika wanasema "hatari hiyo inaonekana kimtazamo zaidi kuliko hali halisi". Sudi Mnette amezungumza na mmoja wa washiriki wa kongamano hilo la wiki moja ambae ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme kutoka Tanzania, Felchesimi Mramba ambae anaanza kwa kuilezea Ujerumani. Kusikiliza mahojiano hayo bonyeza alama ya kusikiliza masikioni hapo chini.

Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman