1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hillary Clinton amshutumu mgombea mwenzake Barack Obama

P.Martin24 Februari 2008

Seneta Hillary Clinton amemshutumu vikali mpinzani wake Seneta Barack Obama katika mvutano wao wa kugombea kuteuliwa kukiwakilisha chama chao cha Demokratik kwenye uchaguzi wa rais utakaofanywa mwishoni mwa mwaka huu.

https://p.dw.com/p/DCe7
Democratic presidential hopefuls, Sen. Barack Obama, D-Ill., left, and Sen. Hillary Rodham Clinton, D-N.Y., argue a point during a Democratic presidential debate in Austin, Texas, Thursday, Feb. 21, 2008. (AP Photo/LM Otero)
Wagombea urais wa chama cha Demokratik,Seneta Barack Obama(kushoto) na Seneta Hillary Clinton kwenye mdahalo wa Austin,TexasPicha: AP

Zaidi anayo Prema Martin.

Seneta Hillary Clinton alipozungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa mkutano wa hadhara katika jimbo la Ohio,alimshutumu Seneta mwenzake Barack Obama kuwa amesambaza vijarida vya kampeni vinavyopotosha kuhusu sera zake za afya.Amesema,vijarida hivyo ni uwongo mtupu na akamshutumu Obama kuwa anatumia mbinu za chama cha Republikan kugombea kuteuliwa kukiwakilisha chama chao cha Demokratik katika uchaguzi wa rais utakaofanywa mwezi wa Novemba nchini humo.Akishika nakala ya kijarida hicho Clinton akaongezea kuwa Seneta Obama anafahamu kwamba si ukweli kuwa mradi wake wa afya utawalazimisha watu kununua bima ya afya hata ikiwa hawana uwezo wa kufanya hivyo.Akamuambia Obama:

O-TON: CLINTON:

Seneta Barack Obama alijitetea kwa kusema kuwa yale yaliyokuwemo katika vijarida hivyo ni sawa.Akaongezea:

O-TON: OBAMA:

Obama alipozungumza katika hospitali moja mjini Columbus wakati wa kampeni yake katika jimbo la Ohio,alisema mradi wake wa siha utapunguza gharama kuliko ule wa Clinton.Hapo aligusia mada iliyotajwa na Clinton katika shutuma zake. Obama amesema,tofauti kuu iliyokuwepo kati ya mpango wake na ule wa Clinton ni kwamba mradi wa Seneta Clinton utawalazimisha watu kununua bima na yeye anapinga utaratibu huo.

Tangu zilipoanza chaguzi za awali kugombea kuteuliwa kukiwakilisha chama cha Demokrat katika uchaguzi wa rais,Obama ameshinda mara 10 kwa mfululizo na hivi sasa yupo mstari wa mbele.Kwa maoni ya wachambuzi wa kisiasa ni muhimu sana kwa Clinton kushinda katika majimbo tajiri ya Ohio na Texas yatakayopiga kura tarehe 4 mwezi Machi.Hivyo ndio ataweza kuwa na nafasi nzuri ya kubakia katika kinyanganyiro cha kugombea kuteuliwa na chama cha Demokrat kugombea uchaguzi wa rais.

Kambi ya Clinton ikitambua umuhimu wa majimbo ya Ohio na Texas,imeimarisha kampeni zake katika majimbo hayo mawili hasa kuwavutia wapiga kura waliotokea nchi za Marekani ya Kusini.Taangu siku chache za nyuma,mume wa Hillary Clinton,aliekuwa rais wa Marekani Bill Clinton na binti yao Chelsea wameanza kufanya kampeni kuwavutia wapiga kura na hasa wale waliotokea nchi za Marekani ya Kusini.Kwani asilimia 25 ya wapigakura katika jimbo la Texas ni kutoka eneo hilo.

Ikiwa Seneta wa New York,Hillary Clinton atachaguliwa rais katika uchaguzi wa Novemba,basi atakuwa rais wa kike wa kwanza nchini Marekani.Na iwapo Seneta wa Illinois Barack Obama atateuliwa kugombea uchaguzi huo na yeye atamshinda mgombea wa Republikan basi atakuwa rais mweusi wa kwanza nchini Marekani.