1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLebanon

Hezbollah yasema wapiganaji wake wawili wameuawa

19 Agosti 2024

Kundi la Hezbollah limesema hivi leo kuwa wapiganaji wake wawili wameuawa katika eneo la Houla nchini Lebanon kufuatia mashambulizi ya Israel.

https://p.dw.com/p/4jeBf
Lebanon | Shambulizi Beirut
Magari ya kusafirisha wagonjwa yaonekana katika eneo la shambulizi kusini mwa Beirut mnamo Julai 30, 2024.Picha: AFP

Kundi hilo la Lebanon linalofadhiliwa na Iran limesema pia kwamba limefanya mashambulizi ya kulipiza kisasi ya droni kaskazini mwa Israel.

Hizi ni ghasia za hivi punde ambazo zinazidisha hofu ya kuzuka kwa vita vipana zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati.

Hofu hiyo imesababisha mashirika ya ndege ya nchi za Magharibi kusitisha safari zao.

Hayo yanajiri wakati vita vya Gaza vikiendelea huku mamlaka za Afya zinazodhibitiwa na Hamas zikisema kuwa idadi ya vifo imefikia watu 40,139.

Duru nyingine ya mazungumzo ya usitishwaji mapigano inatarajiwa kuanza wiki hii mjini Cairo, Misri.