1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLebanon

Hezbollah yadai kushambulia kambi ya jeshi ya Israel

6 Oktoba 2024

Hezbollah imedai kushambulia kwa ndege zisizo na rubani kambi ya kijeshi ya Israel karibu na mji wa kaskazini wa Haifa leo Jumapili.

https://p.dw.com/p/4lSsx
Lebanon | Mashambulizi ya anga ya Israel huko Beirut
Moto na moshi watanda baada ya shambulio la anga la Israel huko Dahiyeh, Beirut, Lebanon. Picha: Hussein Malla/AP Photo/picture alliance

Hezbollah imedai kushambulia kwa ndege zisizo na rubani kambi ya kijeshi ya Israel karibu na mji wa kaskazini wa Haifa leo Jumapili.

Haya yanajiri wakati Israel ikisema imelenga vitongoji vya kusini mwa Beirut, katika operesheni yake dhidi ya kundi la hilo.

Soma pia: Israel yashambulia vikali Hezbollah mjini Beirut

Umoja wa Mataifa unasema mgogoro mkubwa unaendelea Lebanon huku watu wakikimbia makaazi yao kutokana na mashambulizi ya anga.

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, Filippo Grandi amesema mashambulizi mengi dhidi ya Lebanon yanakiuka sheria ya kimataifa ya haki za binaadamu.

Haya yakijiri serikali ya Lebanon imesema imepokea msaada wa tani 25 za dawa na vifaa vya matibabu kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto UNICEF.

Soma pia: Mashambulizi ya Israel yaharibu barabara ya Lebanon-Syria

Waziri wa Afya Firass Abiad leo Jumapili amesema msaada wa UNICEF ni muhimu na utawezesha hospitali kuendelea kutoa huduma.

Mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa tayari yametuma vifaa vya matibabu nchini Lebanon, ambapo Israel kwa sasa inafanya mashambulizi ya ardhini dhidi ya Wanamgambo wa Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran.