1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Hezbollah yaahidi kulipiza kisasi baada ya kuuliwa Nasrallah

28 Septemba 2024

Kundi la Hezbollah nchini Lebanon limeahidi kupigana vita dhidi ya Israel na kuendelea kuiunga mkono Gaza na Palestina, na kuilinda Lebanon na watu wake.

https://p.dw.com/p/4lC6H
Jeshi la Israel lilisema Hassan Nasrallah aliuawa katika shambulizi ''sahihi'' la anga wakati wa mkutano wa viongozi wa kundi hilo kwenye makao yake makuu huko Dahiyeh, kusini mwa Beirut
Jeshi la Israel lilisema Hassan Nasrallah aliuawa katika shambulizi ''sahihi'' la anga wakati wa mkutano wa viongozi wa kundi hilo kwenye makao yake makuu huko Dahiyeh, kusini mwa BeirutPicha: Majid Asgaripour/WANA/REUTERS

Nasrallah aliuwawa kufuatia mashambulizi ya Israel usiku wa kuamkia leo kusini mwa mji wa Beirut. Taarifa ya jeshi la Israel imesema kuwa Ali Karaki kamanda wa Hezbollah anayehusika na kusini mwa Lebanon, pia aliuawa.

Iran, Iraq na Uturuki tayari zimelaani vikali mashambulizi hayo ya Israel nchini Lebanon. Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amesema Marekani haiwezi kukanusha kuhusika kwa sehemu na kifo cha Nasrallah. Hamas imesema inaomboleza kifo cha Nasrallah. Huku waasi Wahuthi wa Yemen wakisema wanadhamiria kupigana na Israeli baada ya mauaji ya Nasrallah.

Jeshi la Israel limesema kwamba kifo cha Nasrallah, kimeufanya ulimwengu kuwa salama zaidi.