1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAMBURG : Beck achaguliwa tena kuongoza SPD

27 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7CT

Chama cha Social Demokratik nchini Ujerumani kimemchaguwa tena mwenyekiti wake Kurt Beck kwa kauli moja.

Beck ambaye alikuwa mgombea pekee wa wadhifa huo alijizolea zaidi ya asilimia 95 ya kura zilizopigwa kwenye mkutano wa chana hicho cha SPD mjini Hamburg.Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter-Steinmeier,Waziri wa Fedha Peer Steinbrück na Andrea Nahles wamechaguliwa kuwa manaibu wake.

Kwa upande wake Steinmeier amekitakia chama hicho kwa kupitia mkutano huo wa chama kuzidi kushikamana na kuwa wazi kwa umma hatua ambayo itawafanya waaminike zaidi.

Chama hicho pia kimepiga kura kuunga mkono pendekezo la Beck kuitaka serikali kuwaruhusu watu wenye umri uliopindukia miaka 50 kuchukuwa marupurupu ya ukosefu wa ajira kwa miaka miwili kamili badala ya miezi kumi na minane ya hivi sasa.

Pendekezo hilo linaonekana kama ni juhudi za Beck kukitenganisha chama cha SPD na washirika wao wenza kwenye serikali ya mseto chama cha Christian Demokratik cha Kansela Angela Merkel nchini.