Hamasa inapanda kuelekea uchaguzi Uturuki
20 Juni 2018Siku chache kabla ya uchaguzi ambao rais Tayyip Erdogan amelazimisha kuufanya nchini Uturuki kujiimarisha katika madaraka , mjadala mkali katika majukwaa ya kijamii unahusika na picha ya mbwa mweusi kilema ambaye nyayo zake zilikatwa na kutupwa.
Watu wengi wameshitushwa na kitendo hicho cha kikatili. Lakini pamoja na kila kitu siku hizi, hata mjadala huu ulichukua mtazamo wa kisiasa. Waungaji mkono wa serikali wamepuuzia jinsi watu walivyokuwa wakijadili suala hilo na kusema ni fadhaa, wakati upinzani umesema ukatili umekuwa jambo la kila siku nchini Uturuki baada ya miaka 16 ya chama cha Erdogan cha Haki na maendeleo AKP kuwapo madarakani.
Kutoka siasa kali za mrengo wa kulia hadi siasa kali za mrengo wa kushoto, watu nchini Uturuki wanajiweka mbali na mfumo wa sasa wa kisiasa. Kwa miaka mingi, wamekuwa wakitambua kwamba utawala wa kimabavu haziishii kwa kupora madaraka ya nchi na kuvunja mfumo wa kisiasa. badala yake zinaendelea kushambulia na kujaribu kuteka nyoyo za binadamu, kuingilia kila sehemu ya maisha ya kila siku kwa sumu yake ya maadili yenye mabovu.
Inalazimisha hali ya kutokuwa na sheria na ukatili mkubwa na kudai utii bila shuruti pamoja na kufuata dini kwa viongozi wake.
Katika mitandao ya kijamii, sehemu pekee ambako Waturuki wanaweza bado kutoa sauti zao na kusikika, mjadala halisi sio juu ya mbwa huyo mweusi. Ni juu ya nia ya kuendeleza akili timamu, kuimarisha maadili ya kiutu katika nchi hiyo, kinyume na kufanywa kuwa watu wenye utii tu.
Matumaini katika uchaguzi
"Ni matumaini ambayo yanachosha , sio maumivu," niliwahi kuandika katika taarifa moja. Na maneno haya yamekuwa maarufu tena katika mitandao ya kijamii. Kwasababu watu wa Uturuki, kutoka kila upande wa uwanja wa kisiasa, wana matumaini katika matokeo ya uchaguzi wa Juni 24.
Matokeo hayo yanaweza kuweka matumaini yao hai kila wakati, licha ya kutambua kwamba matokeo ya uchaguzi huo yataghushiwa tena, ni juu ya hamasa na hisia za upinzani, ambazo zimekuwa zikipiga ngumi mezani kwa nguvu zaidi kuliko wakati mwingine.
Mgombea wa chama cha Social Democratic Muharrem Ince, anachemka kwa joto la hamasa katika mikutano yake mikubwa, kiongozi wa chama cha kizalendo , Meral Aksener, anapambana na erdogan kwa kutoa hotuba kali kali,kiongozi wa chama ambacho kwa kiasi kikubwa ni cha wakurdi cha HDP , Selahattin Demirtas, ana fanya kampeni akiwa katika chumba chake alimofungwa jela, ambako amewekwa kama mfungwa wa kisiasa tangu miezi 20 iliyopita. Na hata chama cha kihafidhina cha Kiislamu kinazungumza lugha ya mshikamano dhidi ya kutokuwa na haki.
Tangu walipojiunga pamoja dhidi ya Erdogan, vyama vyote vimekuwa vikipambana kana kwamba hakuna kesho. Ujumbe wao ni kwamba hakuna mustakabali wa baadaye iwapo watapoteza uchaguzi kwa utawala wa mtu mmoja.
kuweka matumaini yao juu, watu wa Uturuki wamevumilia kila aina ya uchafu kisiasa ambao unaendelea kuja wakati uchaguzi unakaribia. Kuvuja kwa picha ya hotuba ya Erdogan katika mkutano wa ndani wa chama chake ambako alitoa wito wa kukamilisha uchaguzi kabla ya kura kuhesabiwa, kwa "kuweka mbinyo katika masanduku ya kura".
Ripoti za waungaji mkono wa serikali kubeba bunduki wakati wakienda kwa wapiga kura kuwaomba wakipigia chama kilichoko madarakani, katika maeneo ya wakurdi. Kuwatisha wapiga kura na kughushi uchaguzi, kusambaa kwa taarifa za uongo kutoka vyombo vikuu vya habari, kushambuliwa kwa wanasiasa wa Kikurdi, yote hayo yanapuuziwa na serikali.
Mwandishi: Temelkuran, Ece /ZR/ Sekione Kitojo
Mhariri: Yusuf Saumu