1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas yampoteza kamanda wa ngazi za juu

17 Oktoba 2023

Tawi la kijeshi la kundi la Hamas, Al-Qassan Brigades, linasema shambulizi la kutokea angani la Israel limemuua mmoja wa makamanda wake wa cheo cha juu kabisa, Ayman Nofal.

https://p.dw.com/p/4XeSq
Gazastreifen Rafah | Hamas-Kommandeur Ayman Nofal
Kamanda wa Al Qassam Brigades, Ayman Nofal, aliyeuawa na mashambulizi ya Israel.Picha: Ashraf Amra/AP/Zuma/picture alliance

Nofal ndiye mwanamgambo wa Hamas wa ngazi ya juu kabisa kuuliwa kufikia sasa katika harakati ya mashambulizi ya mabomu ya Israel katika Ukanda wa Gaza.

Soma zaidi: Israel, Hamas zaelekea kwenye mgogoro mkubwa Gaza

Israel yaushambulia Ukanda wa Gaza

Kundi la Hamas limesema katika taarifa yake kwamba Nofal, anayejulikana kwa jina Abu Mohammed, ameuwawa leo katika shambulizi lililoilenga kambi ya Bureij katikati ya Ukanda wa Gaza.