Hali ya kisiasa Visiwani Zanzibar kabla ya uchaguzi mwakani
4 Agosti 2009Matangazo
Watu jana na leo katika wilaya
ya uchaguzi ya Ole, Kisiwani Pemba, wakisusia kujiandikisha na
kupinga sharati kwamba lazima wawasilishe vitambulisho vya ukaazi
wa Zanzibar kabla ya kuandikishwa. Fujo zilitokea. Leo tume ya
uchaguzi huko Pemba ililazimika kusitisha zoezi hilo katika eneo hilo.
Punde hivi Othman Miraji alizungumza kwa simu na mwandishi wa habari Munir Zakaria aliyekuweko katika eneo hilo na kumuomba atuarifu nini hasa kilichojiri huko Ole.
Mwandishi: Othman Miraji
Mhariri: Mohamed Abdulrahman