1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haaland arejea tena Dortmund ikiizaba Bremen 4-1

19 Aprili 2021

Mshambuliaji wa Erling Haaland hatimaye alifunga mabao mawili katika ushindi wa Dortmund wa 4 – 1 dhidi ya Werder Bremen na kuyafufua matumaini yao ya kufuzu katika Ligi ya Mabingwa msimu ujao

https://p.dw.com/p/3sEne
Fussball Bundesliga - Borussia Dortmund vs. Werder Bremen
Picha: Leon Kuegeler/AFP

Bayern wanaongoza ligi na pengo la pointi saba dhidi ya nambari mbili Leipzig ambao walilazimishwa sare tasa na TSG Hoffenheim. Wolfsburg bado ipo nafasi ya tatu na pointi 54 pointi moja dhidi ya nambari nne Frankfurt. Erling Haaland hatimaye alifunga mabao mawili katika ushindi wa Dortmund wa 4 – 1 dhidi ya Werder Bremen na kupunguza mwanya kati yao na nafasi ya kufuzu Ligi ya Mabingwa. Msikilize Marco Reus nahodha wa BVB "Nadhani kila mmoja anaweza kusoma jedwali. kila mmoja anafahamu tuko nyuma kwa pointi ngapi. Tuna mechi tano zilizobaki sasa, pointi nne na tano nyuma, kwa hiyo nadhani kila kitu bado kipo wazi. Tulisema lazima tushinde mechi zote sita zilizobaki. Sasa tumeshinda mbili na sasa tutacheza Jumatano dhidi ya Union, na kama bado tunataka kufuzu katika Champions League, basi lazima tushinde mechi zetu zote."

Dortmund ilinufaika na kichapo ilichopata cha timu iliyo katika nafasi ya nne Eintracht Frankfurt mikononi mwa Borussia Moenchengladbach cha 4 – 0. Sasa wana pengo la pointi tano huku zikiwa zimesalia mechi tano msimu kukamilika.

Kocha wa Frankfurt Adi Hutter ambaye alitangaza kuwa atahamia Gladbach kuchukua mikoba ya Marco Rose anayekwenda zake Dortmund msimu ujao, alisikitishwa na kipigo hicho kutoka kwa mwajiri wake wa usoni…

AFP/DPA/AP/Reuters