1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guyana yaomba kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la UM

8 Desemba 2023

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepanga kukutana kwa dharura kwa ombi la Guyana baada ya Venezuela kupiga kura ya maoni kudai udhibiti wa eneo lenye utajiri wa mafuta na madini, la Essequibo.

https://p.dw.com/p/4ZudG
Essequibo, eneo linalozozaniwa na Guyana na Venezuela.
Essequibo, eneo linalozozaniwa na Guyana na Venezuela.Picha: Martin Silva/AFP

Katika barua kwa rais wa baraza hilo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Guyana, Hugh Hilton Todd, ameishutumu Venezuela kwa kukiuka Mkataba wa Umoja wa Mataifa kwa kujaribu kulichukua eneo lake.

Soma zaidi: Djibouti yaiomba UN kumaliza mzozo na Eritrea

Mvutano wa kidiplomasia juu ya eneo hilo umepamba moto tangu mwaka 1962 baada ya Venezuela kupinga makubaliano ya mipaka baina yao ya mwaka 1899 na kuongezeka mwaka 2015 baada ya kampuni ya mafuta ya ExxonMobil kutangaza ugunduzi wa kiasi kikubwa cha mafuta katika pwani yake.

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela tayari ameyaagiza makampuni ya serikali kuanza mara moja utafutaji wa mafuta kwenye eneo hilo.