1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres atafuta kunusuru makubaliano ya usafirishaji nafaka

Sylvia Mwehozi
9 Septemba 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anajaribu kufanya mawasiliano na Urusi katika juhudi za kuyafufua makubaliano ya usafirishaji wa nafaka.

https://p.dw.com/p/4W8Za
Indien, Neu-Delhi | Antonio Guterres gibt Pressekonferenz vor G20-Gipfel
Picha: Anushree Fadnavis/REUTERS

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anajaribu kufanya mawasiliano na Urusi katika juhudi za kuyafufua makubaliano ya usafirishaji wa nafaka. Ujumbe wa viongozi wa Afrika kuwasilisha mpango wa amani kwa marais wa Ukraine na Urusi.

Katika barua ambayo shirika la habari la Ujerumani dpa limeiona, Guterres ametuma mapendekezo kwa waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov ya kulegeza baadhi ya vikwazoikiwa ni pamoja na kuirejesha tena Moscow kwenye mfumo wa kimataifa wa malipo wa SWIFT.

Nakala hiyo inaeleza mapendekezo yatakayowezesha Urusi kufanya mauzo ya mbolea yake na bidhaa za kilimo, ikiwemo kufunguliwa kwa mali za makampuni ya mbolea Ulaya na kuziruhusu meli za Urusi kufikia bandari za Ulaya. Umoja wa Mataifa unatumai kwamba mapendekezo yote hayo yataishawishi Moscow kurejea kwenye makubaliano ya usambazaji wa nafaka baada ya kujiondoa mwezi Julai.